Dodoma FM

Wakazi wa Makutupa wakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama

12 October 2022, 12:17 pm

Na; Na ;Victor Chigwada.

Wakazi wa kijiji cha Makutupa wilayani kongwa wameendelea kutumia maji yasiyo safi na salama licha ya uwepo wa juhudi za  uongozi wa kata ya ngomai kukabiliana na changamoto hiyo.

Hali hiyo imesababisha uwepo  matumizi ya maji ambayo siyo safi na salama hususani katika kipindi hiki cha kiangazi

Mwenyekiti wa kijiji cha Makutupa Bw.Peter Mwachahe amezungumza na Taswira ya Habari ambapo amesema  kuwa maji yanayotumia na wananchi ni yale ambayo yamechanganyika na tope hali ambayo ni hatari kwa afya zao

.

Naye Diwani wa Kata ya Njoge Bw.Abdala Dedu amesema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo  ambapo tayari wapo kwenye  mchakato wa kuchimba kisima cha maji katika Kata jirani ili kusaidia kuyasukuma maji ili kuelekeza kata ya njoge

.