Wananchi jijini Dodoma wanaendelea kuhamasishwa kujitokeza kupata chanjo ya uviko 19
25 August 2021, 1:17 pm
Na; Benard Filbert.
Halmashauri ya jiji la Dodoma inaendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kupata Chanjo ya uviko 19 kwa hiyari lengo ikiwa kukabiliana na ugonjwa huo.
Hayo yameelezwa na afisa afya wa jiji la Dodoma Abdala Mahiya wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu hamasa ya watu kujitokeza katika maeneo yaliyopangwa kupata chanjo ya uviko 19.
Amesema licha yakuwepo kwa vituo vya moja kwamoja ambavyo vinatoa huduma hiyo wameanza kutembea baadhi ya maeneo yenye watu wengi kuhakikisha wanawafikia wananchi kwa ukaribu ikiwepo vituo vya mabasi ili kuwaamasisha kuchanja.
Kadhalika amesema pamoja na chanjo ambayo inatolewa na serikali katika maeneo mbalimbali nchini amewaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zakujikinga na ugonjwa huo na sio kutegemea chanjo pekee.
Jamii inasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na uviko 19 kwa kufuata maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na serikali kupitia wizara ya afya ili kukabiliana na ugonjwa huo.