Uvunaji hafifu wa mahindi wapelekea tishio la njaa kwa baadhi ya familia
9 May 2023, 4:51 pm
Mkoa wa Dodoma ulijiwekea malengo ya kulima hekta 7 za chakula lakini mvua hazikunyesha kama ilivyotarajiwa hivyo kuathiri upatikanaji wa chakula kama ilivyotarajiwa kuilazimu Serikali kutoa mahindi ya bei nafuu jumla ya tani 12,747.15.
Na Mindi Joseph.
Uvunaji Hafifu wa zao la Mahindi katika msimu huu wa Mavuno unatajwa kusababisha upungufu wa chakula kwa baadhi ya Familia Mkoani Dodoma.
Hali hii imechangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa na mvua za kusuasua wakati wa kilimo huku jua likiwaka na kukausha zao hilo.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha makag’wa na hapa wanasema.
Pamoja na uzalishaji kuwa Duni Diwani wa kata ya makag’wa Solomoni Samwel amewahimiza wanachi kuhifadhi chakula ambacho wanavuna.