Madereva wa daladala walia na hali mbaya ya biashara
24 March 2023, 4:30 pm
Awali madereva hao walikuwa wakifanyia biashara za uasafirishaji katika kituo cha sabasaba kabla ya kuahamishiwa katika kituo kipya cha machinga Complex .
Na Thadey Tesha.
Baadhi ya madereva wa daladala jijini Dodoma wamesema kuwa licha ya serikali kuwahamishia katika kituo kipya cha daladala katika eneo la bahiroad jijini hapa bado hali ya biashara si ya kuridhisha.
Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya madereva wa daladala katika eneo hilo ambapo wamesema kuwa utofauti kati ya kituo cha sabasaba na kituo walipo hivi sasa ni ubora wa mazingira lakini mzunguko wa biahara si wa kuridhisha kama awali.
Aidha wameiomba serikali kuweka utaratibu mzuri wa vituo vya kupakia na kushushia abiria ili kutoa uelewa kwa madereva hao ili kuepuka changamot inayopelekea kuweza kukamatwa na askari wa barabarani.