Mashekhe watakiwa kufanya kazi kwa weledi
20 February 2023, 4:20 pm
Baadhi ya mashekhe wa kata wameshindwa kuwa na fikra ya utatuzi wa baadhi ya changamoto katika jamii ikiwemo masuala ndoa, migogoro ya kifamilia na kuwa na njia ya kuhakikisha ofisi za kata zinapatikana
Na Seleman Kodima.
Baraza la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Dodoma Mjini limeendelea kupigilia msumaria kauli ya Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally kuwa haitoweza kuwavumilia mashekhe watakaoshindwa kuhudumia jamii na serikali .
Kauli ya Mufti Mkuu wa Tanzania inawapa nafasi Bakwata kutoweza kuvumilia na kufanya kazi na mashekhe wasioweza kwenda na kasi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Bakwata wilaya ya Dodoma Bashiru Ally Hussein wakati akizungumza hatua ya utekelezaji juu ya kauli ya Mufti Mkuu wa Tanzania ambayo inasema badilikia, jitambue acha mazoea, amesema kauli hiyo inawapa nafasi Bakwata kutoweza kuvumilia na kufanya kazi na mashekhe wasioweza kwenda na kasi ya kuhuduma jamii.