TARURA kutatua changamoto ya barabara Chamwino
2 February 2023, 10:46 am
Wakala wa barabara vijiji na mijini Tarura inatarajia kutatua changamoto ya barabara wilayani Chamwino kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024.
Na Seleman Kodima.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Chamwino imesema inatarajia kutatau changamoto ya Miundombinu ya Barabara katika wilaya ya Chamwino kwa asilimia 200 kupitia bajeti ya mwaka 2023/24 ambayo itagharimu bilion 4.48 .
Akizungumza na Taswira ya Habari Meneja wa TARURA wilaya ya Chamwino Mhandisi Nelson Maganga amesema Bajeti hiyo itaongezeka ikiwa ni sambamba na ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na fedha nyingine.
Amesema Fedha hizo zimegawanyika katika makundi matatu ,ambapo zipo fedha za matengenezo kiasi cha Shilingi billioni 1 milion 489 .