Wakazi wa kisisi walazimika kutumia maji ya visima vya asili
10 May 2022, 4:10 pm
Na; Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Kisisi Wilayani Mpwapwa wanalazimika kutumia maji ya visima vya asili kutokana na kukosa huduma ya maji Safi na salama
Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa licha ya kuchota maji ya visima vya asili lakini bado wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo
Bw.Samweli Chihongwe Ni mwenyekiti wa Kijiji hicho ambapo anakiri changamoto hiyo inawalazimu wananchi kutumia maji ambayo so Safi na kuiomba Serikali kuwasaidia kutatua adha hiyo
Aidha Diwani wa Kata hiyo Bw.Tanu Mkanyagwa amesema maji yanayo tumika katika Kata yake ni ya chemichemi pamoja na makorongoni ambayo si Safi na salama
.
Mkanyagwa ameongeza kuwa pamoja na changamoto hiyo lakinia anamshukuru Mbumge wa Jimbo lao Mh.Geoge Malima kwa kuendelea kupambana na changamoto hiyo katika Kata yao
.
Matumizi ya maji ya visimani si salama kwa afya za watumiaji ukizingatia jamii nyingi za vijijini hazina elimu juu ya kutumia maji yaliyo chemshwa na kuchujwa ili kuua vijidudu