Elimu ya mipaka itolewe kwa viongozi wa mitaa
5 May 2022, 7:40 am
Na;Yussuph Hassan.
Elimu ya mipaka ya ardhi katika kipindi cha Sensa ya watu na makazi imetajwa kuwa muhimu katika kuhakikisha kila eneo linafahamu kwa kina mipaka yake.
Akizungumza na kituo hiki Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nzije Jijini hapa Godfrey Samweli amesema kuwa licha kuwepo kwa ramani za Mitaa, bado kumekuwepo na utata katika baadhi ya mipaka ya ardhi.
Ameongeza kuwa katika eneo lake mipaka anaifahamu vyema huku akisubiria zoezi la sensa ya watu na makazi ifanyike.
.
Kwa upande mwingine baadhi ya wakazi wa Mtaa huo wameonekana kutofahamu umuhimu wa zoezi la sensa ya watu na makazi licha ya kushiriki kwa mara kadhaa sasa.
.
Wameishauri Serikali kutumia vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha elimu inawafikia watu wengi zaidi ili kurahisisha zoezi hilo litakapoanza.
.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti 2022. Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012, Hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ya Sita kufanyika nchini.