Viongozi watakiwa kuwa mstari wa mbele kuhimiza usafi katika maeneo
31 January 2022, 4:02 pm
Na ;Thadei Tesha.
Baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema ili kuhakikisha suala la usafi linapewa kipaumbele katika mitaa mbalimbali ya jiji viongozi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhimiza suala hilo.
wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema viongozi wanao nafasi kubwa katika kuhimiza suala la usafi katika jamii ili kuleta hamasa zaidi kwa wananchi kufanya usafi kwa lengo la kuepukana na magonjwa yatokanayo na mazingira machafu.
Aidha baadhi ya wakazi jijini hapa wamempongeza mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri kwa kuendelea kuhamasisha pamoja na kushiriki zoezi la usafi katika kata ya kikuyu jijini hapa ambapo itaendelea kuleta chachu kwa wananhi kuzidi kufnya usafi.
Akizungumza akiwa katika zoezi la kufanya usafi Mh.Jabir Shakimweri aliwataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ambapo pia amesema wataendelea kuhakikisha wananendelea kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika mitaa hiyo kwa lengo la kutokomeza uhalifu.
Suala la kufanya usafi limekuwa likihimizwa na viongozi mbalimbali ambapo lengo lake ni kuhakikisha wanapunguza magonjwa pamoja na kuweka mazingira kuwa na mvuto katika jamii.