Wananchi waaswa kutunza barabara
2 February 2021, 12:30 pm
Na,Thadey Tesha,
Dodoma.
Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kutunza miundombinu ya barabara zinazoendelea kujengwa katika mitaa mbalimbali ili zidumu na kuwasaidia katika kujiletea maendeleo.
Wito huo umetolewa na mratibu kutoka wakala wa barabara mijini na vijjini TARURA Mkoa wa Dodoma Bw.Lukaso Kilembe wakati akizungumza na Dodoma Fm, ambapo amesema kila mwananchi anao wajibu wa kulinda miundombinu ya barabara iliyojengwa kwa gharama kubwa.
Amewaonya baadhi ya wanunuzi wa vyuma chakavu kuacha mara moja kununua vyuma vinavyotokana na barabara badala yake wakiletewa watoe taarifa kwa mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa, wamekiri kuwepo kwa uharibifu wa miundombinu ya barabara ambapo wameitaka Serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii, ili kila mtu awe mlinzi wa miundombinu hiyo.