Sita wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za wizi
12 January 2021, 1:23 pm
Na,Zakia Ndulute,
Dodoma.
Mahakama ya Hakimu Wilaya ya Dodoma imewapandisha kizimbani washtakiwa sita wakazi wa Dodoma kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mahakama imemshikilia Mtuhumiwa PIUS JOSEPH YOHANA (20), ALOYCE ISSACK(18), LUCK PAULO(18), RAMADHANI MUSA(20), MUSTAPHA ABUU(20) pamoja na ONESMO KAMGISHA(23) wote wakidaiwa kutenda kosa moja.
Wakisomewa Shitaka lao mbele ya Hakimu Wilaya ya Dodoma MARRY INNOCENT SENAPEE na mwendesha mashtaka wake ambaye ni wakili wa Serikali HARRY MBOGORO amedai kuwa mnamo Novemba 2 mwaka 2020 washitakiwa wote kwa Pamoja waliiba computa mpakato yenye thamani ya shilingi elfu sabini flashi ya shilingi ya elfu ishirini mashine ya umeme ya shilingi laki tatu na Modem ya Vodacom ya shilingi elfu 70 Adapta chaji ya shilingi elfu 30 na simu ya chaja ya shilingi elfu 15pamoja na begi moja la komputa mpakato lenye thamani ya shilingi elfu 30 na mali zote hizo zikiwa ni za ROBERT MATONYA vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja laki moja na elfu sitini na tano.Wakili ameongeza kuwa washitakiwa walifanya tukio hilo katika eneo la Nkuhungu Ndani ya Wilaya ya dodoma na baada ya kuiba walimpiga mmiliki wa vitu hivyo na kisha kuchukua mali zake na kuondoka nazo kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Hata hivo washitakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo ,Naye wakili wa Serikali amesema kuwa upelelezi umekamilika na kumuomba Hakimu ataje tarehe ya kusikilizwa tena kwa kesi hiyo mahakamani
Kwa upande wake Hakimu SENAPEE amesema kuwa kosa hilo halina dhamana na washitakiwa warudishwe rumande chini ya uangalizi wa Jeshi la Magereza na shauri lao litasikilizwa tena januari 18 mwaka huu.