Sheria ya ndoa jinsi inavyo leta mkanganyiko kwa jamii
2 August 2021, 1:46 pm
Na; Benard Filbert.
Serikali imeombwa kuangalia upya sheria ya ndoa ya mwaka 2002 ambayo inamruhusu mtoto wa kike kuoelewa chini ya miaka 18 kwani imekuwa ikileta mkanganyiko katika jamii huku baadhi yao wakilazimika kukatisha masomo yao.
Hayo yameelezw na Emmanuel Emoshi ambaye ni mwanasheria kutoka shirika lisilo la kiserikali Action For Community Care ambalo limekuwa likijihusisha na haki za binadamu.
Bwana Emoshi amesema serikali inajitahidi kuboresha sheria mbambali lakini baadhi zimekuwa zikikinzana ikiwepo sheria ya ndoa ya mwaka 2002 ambayo kuna kifungu kinaruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18.
Amesema sheria ya ndoa pamoja na sheria ya mtoto ni vyema zikaangaliwa vizuri ili kujua namna gani zinaweza kusimamiwa ipasavyo ili kuepusha mkanganyiko katika jamii.
Mmoja wa mzazi akizungumza na taswira ya habari amesema ni kweli sheria hizo zinatakiwa kubadilishwa ili kuepusha mkanganyiko katika jamii.
Sheria ya ndoa ya mwaka 2002 inamruhusu mtoto wa kike mwenye miaka 15 kuolewa kwa idhini ya wazazi na mwenye miaka 14 kwa idhini ya mahakama.