Wachambuzi wa sera watarajia kukutana na wadau wa kilimo
2 August 2021, 1:12 pm
Na; Mariam Matundu.
Kikundi cha wachambuzi wa sera na Wadau wa kilimo wanatarajia kukutana katika kongamano la saba la mwaka kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuongeza tija katika sekta hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kikundi cha wachambuzi wa sera Audax Rukonge amesema katika kongamano hilo watajikita zaidi kujadili ushindani wa bidhaa za kilimo katika masoko ya kikanda na masoko ya nje .
Nae Jackiline Mkindi mkurugenzi mtendaji wa TAHA na mwenyekiti wa baraza la kilimo amesema ni wakati sasa sekta binafsi zikapanua mjadala zaidi ya kutengeneza mazingira wezeshi ya biashara katika sekta ya kilimo ili kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo.
Kwa upande wake mshauri wa sera ,chuo kikuu cha jimbo la Michigan Prof David Nyange amesema pamoja na kutafuta suluhu katika sekta ya kilimo ni muhimu pia kuitazama sekta ya viwanda kwakuwa sekta hizo zinaenda sambamba .
Bwana Gungu Mibavu ni kaimu mkurugenzi wa sera na mipango kutoka wizara ya kilimo amesema wanatumia jukwaa hilo kufanya uchambuzi wa mambo yanayotekelezwa na wizara pamoja na kupata maeneo mapya ambayo yanachangamoto.
Kikundi cha wachambuzi wa sera watakutana katika kongamano la saba la mwaka kwa siku tatu kuanzia tarehe tatu hadi tano mwezi wa nane mwaka huu jijini Dodoma ,kongamano litakalo wakutanisha zaidi ya washiri miambili kutoka katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi pamoja na wadau wengine.