Akina mama wajawazito watakiwa kuzingatia lishe bora ili kuepuka kujifungua mtoto mwenye tatizo la mdomo wazi
29 July 2021, 10:52 am
Na; Benard Filbert.
Akina mama wajawazito wameshauriwa kuzingatia lishe bora kwa kil mlo ili kuepuka kujifungua mtoto mwenye matatizo ya mdomo wazi.
Ushauri huo umetolewa na daktari kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) daktari Peter Mabula wakati akizungumza na Dodoma FM kuhusu tatizo la mdomo wazi katika jamii.
Daktari Peter amesema tatizo la mdomo wazi/mdomo sungura ni kubwa katika jamii hivyo zinatakiwa juhudi binafsi ili kuzuia wakina mama kujifungua mtoto mwenye tatizo hilo.
Amesema asilimia kubwa ya tatizo la mdomo wazi ni vina saba na haliwezi kuzuilika kitaalamu lakini kwa asilimia 5 hadi 7 linaweza kuzuilika hususani kwa mwanamke mjamzito kuzingatia lishe bora.
Amesema katika maeneo ya Vijijini tatizo la mdomo sungura ni kubwa kutokana na ukosefu wa elimu na kujua namna ya kupangilia lishe bora kutokana na maisha duni.
Mmoja kati ya wanawake katika jiji la Dodoma akizungumza na taswira ya habari amesema baadhi ya wanawake wajawazito wamekuwa na desturi ya kuto kuhudhuria clinic hali inayopelekea kukosa elimu ya lishe bora.