Ukosefu wa sera ya unywaji pombe wachangia kuzorotesha uchumi
30 November 2020, 7:22 am
Kutokuwepo kwa sera madhubuti zinazohusu masuala ya unywaji pombe kupita kiasi kumechangangia kushindwa kufanyika kwa shughuli za kiuchumi kutokana na baadhi ya watumiaji wa vinywaji vikali kuendekeza unywaji kupita kiasi.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Mtandao wa mashirika ya kupambana na unywaji pombe kupita kiasi Tanzania TAAnet Sophia Komba wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu namna ya kupunguza madhara yatokanayo na pombe ili kuinua kiwango cha maisha ya watanzania kiafya,kijamii na kiuchumi.
Akifunga mafunzo hayo mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma Mh.Fatma Toufiq amesema waandishi wa habari wanakila sababu ya kuhamasisha upatikanaji wa sera madhubuti ya kupambana na madhara ya unywaji pombe uliopitiliza.
Ameongeza kuwa wangependa kuona watunga sera wanalitafutia ufumbuzi tatizo hilo kwa kuwa na ubunifu ambao utaokoa maisha, kama vile kutokomeza athari zitokanazo na unywaji pombe kupindukia.