Wananchi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani.
6 May 2021, 11:41 am
Na; Mariam Kasawa
Wananchi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya utalii wa ndani katika mbuga mbalimbali ili kufahamu vivutio vingi vya utalii vinavyo patikana hapa Nchini.
Ushauri huo umetolewa na wawakilishi kutoka hifadhi ya Taifa Tanzania TANAPA wakati wakizungumza na Dodoma FM juu ya kampeni ya kutembelea mbuga za wanyama msimu wa sikukuu ya Eid .
Bi. Beatrice Mtambi ni Afisa mwandamizi anaesimamia masuala ya utalii katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire amesema lengo lao ni kuhamasisha wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na viongozi kutembelea katika hifadhi za Taifa Tanzania
Bi. Mtambi ametaja gharama watakazochangia watu zitawapatia huduma ya malazi , chakula pamoja na gharama ya gari la kuwatembeza mbugani ambapo amebainisha gharama hizo kama ifuatavyo.
Amewataka wananchi kuacha kuamini kuwa utalii unafanywa na watu wanao toka nje ya nchi bali wawe na utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii Nchini kwani gharama zake ni nafuu ambazo zinamuwezesha kila mtanzania kumudu .
Wananchi wametakiwa watambue kuwa utalii ni jukumu la kila mtu ndani ya Nchi ili kuweza kujifunza na kuvifahamu vivutio mbalimbali vinavyo patikana ndani ya nchi.