Wananchi watakiwa kuhudhuria kampeni za wagombea kusikiliza sera zao
22 November 2024, 1:04 pm
Ikumbukwe kuwa jumla ya vijiji 12,280, mitaa 4,264 na vitongoji 63,886 ndivyovitakavyoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 .
Na Fred Cheti.
Wananchi wa jijini Dodoma wametakiwa kujitokeza kuhudhuria kampeni za wagombea wa vyama vyote 14 vinavyofanya kampeni katika maeneo yao ili kusikiliza sera zao kabla ya siku ya kupiga kura Novemba 27 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wa uchaguzi jiji la Dodoma Dkt.Fredrick Sagamiko wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake ambapo ametoa taarifa juu ya mambo muhimu kuhusu uchaguzi huo.
Katika hatua nyingine Dkt Sagamiko amewakumbusha viongozi wa vyama vya Siasa kuwakumbusha wagombea wao kutumia vyema majukwaa hayo kufanya kampeni za kistaarabu ambazo hazitaleta uvunjifu wa amani
Miongoni mwa wadau muhimu sana katika mchakato huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU je upi wito wao kwa wagombea na wananchi katika kipindi hiki cha kampeni? Zacharia Mwandumbya ni Mwakilishi wa Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Dodoma anabainisha zaidi
Ikumbukwe kuwa jumla ya vijiji 12,280, mitaa 4,264 na vitongoji 63,886 ndivyo vitakavyoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 ambapo Vyama vya siasa kupitia wagombea wa nafasi mbalimbali wameanza Rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa.