Mradi wa taka rejeshi kuwanufaisha wakazi kata ya Chamwino
22 November 2024, 12:33 pm
Wananchi wamepaswa kutambua kuwa chupa za plastiki ni mali hivyo si vema kuzitupa ovyo na kuharibu mazingira.
Na Fred Cheti.
Majaribio ya Mradi wa uchakataji chupa za plastiki umetajwa kuwanufaisha wananchi wa kata ya Chamwino amabao wengi wamepata ajira kupitia uchakataji wa chupa hizo.
Mara nyingi watu wanapomaliza matumizi ya chupa za plastiki zenye vinywaji au maji huzitupa chupa hizo na kugeuka kuwa takataka bila kujua kuwa chupa hizo bado hubaki na thamani ambayo inaweza kuzalisha pesa kama ambavyo anabainisha Onesmo Kamuruku Mwenyekiti wa Mradi wa uchakataji chupa ujulikanao kama PWP.
Kiongozi Mzuri ni yule ambae anajali maendeleo ya wananchi wake Jumanne ndege ni Diwani wa Kata ya Chamwino yeye amaeiona fursa hiyo na kuwataka wananchi wake hasa vikundi vya taka kuiona kama lulu kwani inaweza kubadilisha taka hizo fursa kubwa ya kiuchumi.
Bwana Suleiman Sanya ni Mwenyekiti wa vikundi vya usafi katika jiji la Dodoma je yeye anasemaje kuhusu fursa hiyo?