Watu wenye ualbino waomba kipaumbele mikopo ya 2%
22 November 2024, 12:08 pm
Mikopo hiyo itawasaidia kazi katika mazingira rafiki na kujikinga na ugonjwa wa saratani ya ngozi .Picha na Steven Noel.
Na Steven Noel.
Watu wenye ualbino wilayani Mpwapwa wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwapa kipaumbele Katika mikopo ya asilimia 2 ili wafanye kazi Katika mazingira rafiki na kujikinga na ugonjwa saratani ya ngozi .
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti Watu Wenye Ualbino Wilaya ya Mpwapwa Alpha Sweda katika zoezi la uchunguzi wa ugonjwa wa saratani ya ngozi na uwagawaji wa vifaa saidizi .
Mathias Jeremia ni kijana mwenye ualbino anasema kutokana na ngozi za kushindwa kumili jua hivyo hushindwa kujishughulisha na shughuli za kilimo ambazo ndio shughuli za Wananchi wengi waishio vijijini na kusababisha kuishi maisha ya umaskini .
Kwa upande wake mratibu wa Afya kutoka shirika lisilo la kiserikali Innocent Mandu amesema wameamua kufanya uchuguz huo Kwa lengo kupunguza tatizo la saratani ya ngozi Kwa watu wenye ualbino.