Dodoma FM

DOWOSA yawaelekeza wanawake ujasiriamali

5 November 2024, 5:57 pm

Na. Anselima Komba

Chama cha Akiba na Mikopo cha Wanawake wa Dodoma (Dodoma Women Saccos Limited) kimejizatiti kuwakwamua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali.

Mhe. Mbonipaye Mpango Mke wa Makamu wa Rais amebainisha hayo wakati wa mkutano mkuu wa pili wa Dodoma Women Saccos Limited mwishoni mwa jana Jijini Dodoma.

Pichani Mhe. Mbonipaye Mpango Mke wa Makamu wa Rais akihutubia wakati wa mkutano wa pili wa DOWOSA
Sauti ya Mhe. Mbonipaye Mpango

Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule Amewapongeza Viongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Wanawake wa Dodoma kwa kuanzisha marubani wa kupunguza changamoto za wanawake kwenye mikopo.

Pichani Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule akiwapongeza Viongozi DOWOSA kwa kuanzisha marubani wa kupunguza changamoto za wanawake kwenye mikopo
Sauti ya Mhe. Rosemary Senyamule

Kitorina Kipa Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Wanawake wa Dodoma amesema malengo ya kuanzisha Saccos hii ni kuwakwamua wanawake kiuchumi kutokana na wanawake wengi wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutokana na kukopa mikopo kwenye baadhi ya taasisi za fedha zenye masharti magumu na Riba kubwa.