Wanafunzi chachu ya mabadiliko katika jamii
11 October 2024, 7:25 pm
Wanafunzi zaidi ya 900 kutoka shule 10 za sekondari Mkoani Dodoma wameshiriki Mdahalo wa kuwajengea uwezo wa kupambana na Rushwa,matumizi ya dawa za Kulevya na kijikinga na Maambukizi ya VVU.
Mdahalo huo umeandaliwa na Takukuru Mkoa kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania,Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora unalenga kujenga jamii isiyo na rushwa.
Akizungumza na wanafunzi Leo Jijini Dodoma Afisa Uchunguzi Kiongozi na kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Zacharia Mwandumbya anasema wanafunzi wa Sekondari wakipata elimu hii itakuwa chachu ya kufanya mabadiliko katika Jamii.
Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki mdahalo huo wameahidi kusimama imara dhidi ya mapambano ya rushwa dawa za kulevya na kujikinga na maambukizi ya Vvu.
Midahalo ya wanafunzi na wanavyuo kuhusu Rushwa mmomonyoko wa Maadali, kupinga matumizi ya dawa za kulevya, kuzuia maambukizi ya VVU na kuhamasisha utawala bora ni endelevu ili Kujenga uadilifu na jamii isiyo na rushwa.