Dodoma yafurahia wiki ya Madaktari Bingwa
23 September 2024, 8:43 pm
Ujio wa Madaktari Bingwa mkoani Dodoma unatajwa kuwasaidia wananchi kupata huduma za kiafya . Wananchi takribani 100,000 wanatarajia kupata huduma za afya kutoka kwa Madaktari Bingwa kwenye Halmashauri 184 kote nchini.
Na Mindi Joseph.
Jumla ya Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia wapatao 50 watahudumia wananchi kwa siku sita kwenye Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyemule amesema kuwa Madaktari hao watafanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.
Mhe. Senyemule amesema hayo wakati wa mapokezi wa Madaktari hao leo 23 Septemba 2024 jijini Dodoma.
Aidha wananchi nao hawakusita kueleza furaha yao kwa ya kupata huduma za afya kutoka kwa Madaktari bingwa watakaokuwa katika hamashauri mbali mbali jijini Dodoma.