Tabiawatu ni chanzo cha uharibifu wa mazingira
9 September 2024, 7:52 pm
Hali ya Mazingira Tanzania inatajwa kuwa mbaya huku Sheria kizani zikichangia.
Na Mindi Joseph. Hali ya Mazingira Tanzania inatajwa kuwa mbaya huku Sheria kizani zikichangia. Tabia watu inasababishwa na shughuli za binadamu zisizo endelevu ikiwemo matumizi ya nishati chafu ufugaji holela na kilimo.
Baadhi ya Wananchi wanasema ipo haja ya serikali kuwekeza utoaji elimu kwa jamii ili kubadili Tabia watu.
Makamu wa Rais Dkt. Mpango, mapema leo hii wakati akifungua Mkutano maalumu wa Viongozi wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu mwelekeo wa Mazingira Nchini amebainisha tabiawatu kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji anasema Lengo la Mkutano huo ni kuongoza juhudi za Kukabiliana na uharibifu wa mazingira.