Kijanisha kunufaisha wakulima milioni 350
8 August 2024, 4:43 pm
Shirika la Justdiggit ambalo kwa Tanzania linashirikiana na Lead Foundation limeanzisha Application hiyo lengo likiwa kutoa elimu bure ili kuwanufaisha wakulima wadogowadogo takribani milioni 350 katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara.
Na Selemani Kodima.
Takriban wakulima wadogo milioni 350 kutoka ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara wanatarajia kunufaika na elimu ya kilimo kupitia Application ya Kijanisha iliyoanzishwa na shirika la Just Digit.
Miezi michache iliyopita, shirika hilo limefanya majaribio makubwa ya app hiyo kwa kushirikiana na mamia ya wakulima wa Tanzania, takribani nchi nzima.
Akizungumza katika uzinduzi huo meneja uhuishaji ardhi kutoka Justdigit Merry Sengelela amewahimiza wakulima, wafugaji na watu wengine kupakua Application hiyo ili kupata elimu.
Naye mkulima kutoka Kijiji cha Mpamantwa Wilayani Bahi Aivan Lungwa ni moja ya wakulima ambao tayari amepakuwa Application hiyo na hapa naelezea uzoefu na faida aliyoipata.