Soko la Hamvu Chang’ombe kunufaisha kiuchumi wakazi 6000
17 July 2024, 5:33 pm
Kata ya Chang’ombe ina wakazi wapatao elfu 39000 na hadi sasa ina soko moja tu linalotumika la Mavunde na kukamilika kwa ujenzi wa soko la Hamvu itaongeza idadi ya masoko mawili.
Na Mindi Joseph.
Kukamilika kwa Ujenzi wa soka la Hamvu katika kata ya chang’ombe imetajwa kunufaisha wananchi zaidi ya Wakazi elfu 6000 kiuchumi.
Huu ni Mtaa wa Hamvu uliopo katika Kata ya chang’ombe Wananchi na wafanyabiashara wa mtaa huu wamezungumzia ujenzi huo.
Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa wa Hamvu Khalid Majid Hamad amewataka wanachi wanaozunguka soko hilo kushiriki kimilifu kufanyabiashara ili kujikwamua kiuchumi.
Je ujenzi wa soko hili utakamilika kama ulivyopangwa Fundi Selemani Msandina anasema.
Diwani wa kata ya Chang’ombe Mh. Bakari Fundikira anasema soko hili litaongeza mapato katika jiji la Dodoma na litawanufaisha wananchi.