Dodoma FM

Waziri Dkt. Jafo awasilisha bajeti 2024/25 leo

23 April 2024, 6:48 pm

Picha ni Mh Dkt. Seleman Jafo akisoma bajeti hiyo leo Bungeni. Picha na Ofisi ya makamu wa Rais.

Hivyo, Waziri Dkt. Jafo ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya shilingi 62,686,762,000 kwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25.

Na Mariam Kasawa.
Ofisi ya Makamu wa Rais inaandaa Mfumo wa Kieletroniki wa Uratibu wa Taarifa za Masuala ya Muungano na yasiyo ya Muungano.

Pia, inaanzisha Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (MAKAVAZI) ili kuwa na mfumo endelevu wa kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za mambo ya Muungano ili kuongeza uelewa wa masuala ya Muungano kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati akiwasilisha Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 leo Aprili 23, 2024.

Akizungumzia mfumo huo amesema lengo ni kurahisisha, upatikanaji, uandaaji, uchambuzi na uunganishaji wa taarifa za utekelezaji wa masuala ya Muungano na yasiyo ya Muungano.

Sauti ya Dkt. Jafo

Picha ni baadhi ya wageni waliokuwepo Bungeni leo wakati bajeti hiyo ikiwasilishwa.Picha na Ofisi ya makamu wa Rais.

Kwa upande wa mazingira, Waziri Jafo amesema Ofisi imeandaa Mradi wa Kuhimili Athari za Mafuriko na Kuongeza Usalama wa Chakula Katika Maeneo yanayoathiriwa na Mafuriko Nchini.

Amesema lengo la mradi huu ni kuijengea uwezo jamii katika kuhimili athari za mafuriko kwa kuwa na shughuli endelevu za kujipatia kipato na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo yaliyoathirika.

Sauti ya Dkt. Jafo