Waumini wa Kikristo watakiwa kuiadhimisha Pasaka kwa kutenda mema
28 March 2024, 8:09 pm
NaThadei Tesha.
Waumini wa dini ya kikristo wametakiwa kuiadhimisha siku ya alhamisi kuu kwa kutenda matendo mema pamoja na kufanya toba.
Wakristo kote ulimwenguni wakiwemo wa kanisa Wakatoliki wanaungana katika kuadhimisha siku ya alhamisi kuu,siku hii ikiwa ni mwendelezo wa kipindi cha kwaresma ambacho kilianza jumatano ya majivu.
Kwa mujibu wa viongozi mbalimbali wa dini hususan kanisa katoliki wanasema kuwa siku hiyo ndio mwanzo wa waumini kufunga na kuanza kipindi cha siku 40.
Lakini je siku hii ina maana gani kwa wakristo?Padre Sostenes Ndedya ni paroko kutoka parokia ya kisasa jijini Dodoma anaeleza.
Na hapa ni katika parokia ya kiwanja cha ndege jimbo kuu katoliki Dodoma ambapo maandalizi ya ibada yanaendelea hapa.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo nao wanaeleza juu ya siku hii.