Wakandarasi watakiwa kuzingatia matakwa ya jiji la Dodoma
31 October 2023, 10:49 am
Huu ni mpango wa Uboreshaji wa Miundombinu katika miji ya Tanzania ujulikanao kama TACTIC unaofanywa na wakandarasi watatu.
Na Fred Cheti.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amewataka wakandarasi waliopewa miradi ya kujenga miundombinu ya barabara katika jiji la Dodoma kuhakikisha wanazingatia matakwa ya jiji la Dodoma kuwa na mpangalio wenye hadhi ya kimataifa.
Mhe Senyamule ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika hafla fupi ya kuanza kwa utekelezaji wa Uboreshaji wa Miundombinu katika miji ya Tanzania ujulikanao kama TACTIC unaofanywa na wakandarasi watatu ambao ni Mkandarasi mkuu CHINA GEO ENGINEERING co. huku mhandisi Msaidizi akiwa ni kampuni ya HONG KONG IK CONSULTANTS CO.LTD kwa kushirikiana na kampuni ya GAUGE Pro. LTD.
Katika hafla hiyo pia alikuwepo Mbunge wa jiji la Dodoma ambapo ameelezea endapo miradi hiyo itafanyika kwa ufanisi itakuwa na manufaa makubwa katika jiji la Dodoma.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe Jabir Shekimweri amewataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kulingana na thamani ya pesa ambayo watapatiwa na si kuleta ujanja katika utekelezaji.
Akizungumza kwa niaba ya wakandarasi wakuu katika ujenzi wa Miradi hiyo…. amesema kuwa watahakikisha wanaitekeleza kulingana na matakwa ya jiji laDodoma pamoja na kuikamilisha kwa wakati.
Sauti ya Mkandarasi.