

10 February 2025, 6:12 pm
Jeshi polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kwa wote wanaojihusisha na uhalifu na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia kijana anaefahamika kama Omar Bakari mwenye 45 kwa kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi wastani wa kilo 148 kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kamanda wa Polisi George Katabazi amebainisha kuwa tukio hilo limetokea Jumanne ya Feb, 4 2025 wilaya ya chemba kwa kutumia gari aina ya mitsubishi canter.
Aidha Kamanda katabazi amebainisha kuwa Jeshi polisi limefanikiwa kuukamata mtandao wa wahalifu maarufu kama maronjoo wanaojihusisha na wizi, uporaji na ubakaji kwa kutumi silaha.