Uhaba wa mbegu za mihogo wawakatisha tamaa wakulima
10 December 2020, 2:33 pm
Na,Mindi Joseph,
Dodoma.
Imeelezwa kuwa gharama kubwa za upatikanaji wa mbegu za zao la mihogo Mkoani Dodoma imechangia baadhi ya wakulima kukata tamaa kulima zao hilo.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wakulima kutoka Hombolo Bwawani Mkoani Dodoma wamebainisha kuwa mbegu za zao la mihongo hazipatikani kwa wakati licha ya zao hilo kustahimili ukame.
Kufuatia changamoto hiyo Taswira ya habari imezungumza na mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wazalishaji wa mbegu bora za mihogo Dodoma Bw,Ipyana Mmota na amebainisha kuwa wanafanya jitihada kubwa za kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo kwa kuendelea kuzalisha mbegu za kutosha ambazo zitawafikia wakulima ili walime zao hilo himilivu.
Aidha imeelezwa kuwa zao la Mihogo limekuwa na tija kubwa kwa baadhi ya wakulima kwani linastahimili ukame na uzalishaji wake umekuwa na manufaa.