Katika juhudi za kukijanisha Dodoma RC Senyamule aongoza wananchi kupanda miti
14 March 2023, 4:21 pm
Kuuendeleza juhudi za kuukijanisha Mkoa wa Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule leo ameongoza wazazi,waalimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Chang’ombe B kupanda miti.
Na Fred Cheti.
Katika kuuendeleza juhudi za kuukijanisha Mkoa wa Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule leo ameongoza wazazi,waalimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Chang’ombe B kupanda miti ya matunda katika eneo la shule hiyo.
Tukio hilo limefanyika mapema leo asubuhi katika shule ya Msingi Chang’ombe B iliyopo kata ya Chang’ombe jijini hapa tukio lililoandaliwa na kamati ya Mazingira katika taasisi ya WANAWAKE NA SAMIA iliyopo jijini dodoma ambapo mkuu huyo wa mkoa amesema kila mkazi wa dodoma anapaswa kutambua umhimu wa kukijanisha mkoa wa dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira katika Mtandao wa WANAWAKE NA SAMIA bi Bhoke Mkami ameeleza lengo la kupanda miti huku jukumu la kutunza miti hiyo likikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Chang’ombe B ameahidi kuhahakisha anaisimamia miti hiyo ili ikue na kuleta manufaa shuleni hapo.
Nao baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wameeleza juu ya zoezi hilo la upandaji wa miti huku wakiahidi kuitunza miti hiyo.