Nzelenze waiomba serikali huduma ya maji safi na salama
1 March 2023, 5:14 pm
Hatua za kukabiliana na changamoto ya maji vijijini bado zinaendelea ili kuondokana na matumizi ya maji yaliyo tuama na visima vifupi ambayo ni hatari kwa afya za binadamu.
Na Victor Chigwada
Wananchi wa kitongoji cha Nzelenze Kata ya Itiso Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuongeza visima vya maji safi na salama ili kuwasaidia kuondokana na matumizi ya maji ya visima vya makorongoni.
Wakizunguma na taswira ya habari miongoni mwa wananchi hao wemesema kuwa shida hiyo imekuwa ikiwalazimu kutembea umbali mrefu kufuata maji ambayo si salama kwao .
Aidha wameomba kusaidiwa na kuongezewa miundombinu ya visima vya maji yatakayo saidia kutatua changamoto hiyo kwa vitongoji amabvyo havina huduma hiyo ya maji.
Diwani wa Kata ya Itiso Bw.Simoni Matambila amekiri changamoto hiyo kuwaathili baadhi ya wananchi wa vitongoji vyake hivyo kupelekea hitaji hilo kuwa kubwa zaidi kwa wananchi
Matambila ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa visima vya maji safi na salama wanachi wanalazimika kutembea umbali mrefu ili kufuata maji ya visima vya kuchimba kwa mkono