Baraza La Taifa la Ujenzi lajipanga kutekeleza Majukumu Tisa
15 February 2023, 11:14 am
Na Fred Cheti.
Baraza La Taifa la Ujenzi limesema kwa Mwaka 2023 limejipanga kutekeleza Majukumu Tisa ambapo ni pamoja na kukamilisha muongozo wa gharama za ujenzi wa barabara Nchini kwa kuandaa gharama za msingi za Mkandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali kwa kila Mkoa Tanzania Bara.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Dkt. Matiko Mturi Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi amesema katika mwaka 2023 Baraza limejipanga kukamilisha muongozo wa gharama za ujenzi ambao utaelezea bei ya vifaa vya ujenzi pamoja na gharama za ujenzi.
Aidha Dkt. Mturi amesema wameandaa mapendekezo ya kuboresha sheria na muongozo wa kusimamia ujenzi wa majengo Nchini na kuhakikisha usalama katika Majengo hasa kwa yale majengo makubwa .