Dodoma FM
Serikali yafanikiwa kupunguza maambukizi ya Malaria Jijini Dodoma
2 February 2023, 1:48 pm
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kupunguza maambukizi ya Malaria kutoka asilimia 1.4 hadi kufikia asilimia 1.01 mwaka 2022.
Na Alfred Bulahya
Hayo yamebainishwa na mratibu wa malaria kutoka halmashauri ya jiji la Dodoma Bw, Gasper Kisenga wakati akizungumza na Taswira ya habari.
Amesema mafanikio hayo yamechagizwa na atua mbalimbali ikiwemo ugawaji vyandarua sambamba na kupuliza dawa kwenye mazalia ya Mbu.
Katika kuendelea kutokomeza ugonjwa huo Dkt Kisenga amesema wamekuja na mpango wa kugawa vyandarua kwa wanafunzi wa shule za msingi huku akikemea suala la watu kupuliza dawa wakati wakiwa ndani ya vyumba vyao.