Ukosefu wa Elimu ya mikopo wakwamisha marejesho Bahi.
28 June 2022, 8:09 am
Na;Mindi Joseph.
Vikundi vya wanawake na watu wenye ulemavu katika halmashauri ya Bahi Mkoani Dodoma vimeshindwa kurejesha mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 58.28.
Chanzo cha kushindwa kurejesha mikopo hiyo kinatajwa kuwa ni kutokuwa na elimu ya ujasiriamali na namna ya kuendesha mikopo hiyo.
Taswira ya habari imezungumza na Mwenyekiti wa halmashauri ya Bahi Donald Mejiti ambaye amesema elimu hutolewa isipokuwa mienendo mibovu ya biashara husababisha vikundi kukwepa kurejesha mikopo hiyo.
.
Kwa upande wake Mkaguzi wa hesabu za Serikali kutoka ofisi ya mkaguzi,Fredrick Magawa ametoa ushauri wa elimu kutolewa mara kwa mara kwa vikundi hivyo.
.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamis Munkunda ameagiza hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu hesabu za serikali [CAG]zifungwe kabla ya Agosti,30,2022.
.
Ikumbukwe kuwa kati ya hoja 87 za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa halmashuri ya Bahi,hoja 22 zimependekezwa kufungwa kwani ziko ndani ya uwezo wa halmashauri.