Halmashauri ya jiji la Dodoma yaanzisha mpango wa kufanya usafi
31 May 2022, 1:16 pm
Na; Fred Cheti
Katika kuendelea kuimarisha usafi wa mazingira jijini hapa halmsahauri ya jiji la Dodoma kwa kushirikiana na wadau mabalimbali wa mazingira imeanzisha mpango wa kufanya usafi siku ya jumamosi katika kata mabalimbali zilizopo jijini hapa.
Afisa Mazingira jiji la Dodoma Bwn. Ali Mfinanga ameelezea lengo la kufanya hivyo ni kuhakiksha jiji la Dodoma linakuwa safi huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao .
.
Daruche Said Mwakilishi wa kikundi cha kutunza Mazingira cha CHAPAKAZI ambapo hapa anelezea moja ya lengo la kikundi chao ni kuhakisha wanayafikia maeneo mbalimbali jijini hapa kwa ajili ya kutoa elimu juu ya kutunza mazingira.
.
Kwa upande wao wadau wengine wa Mazingira jijini hapa nao wametoa maoni yao juu ya suala la kufanya usafi katika jiji la Dodoma.
.
Halmsahauri ya jiji la Dodoma inaendelea kuwasisita wananchi wake kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao ya makazi na biashara kwa kufuata maelekezo na utaratibu uliowekwa na uongozi wa jiji la Dodoma.