Wananchi wa kata ya Ihumwa waanza mchakato wa ujenzi wa vyumba vya madarasa
19 May 2022, 3:20 pm
Na; Victor Chigwada.
wananchi wa Kata ya Ihumwa wilaya ya Dodoma mjini wameanza kuchukua jitihada za kuanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kutokana na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi Ihumwa A .
Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa wingi wa wanafunzi katika chumba kimoja unapunguza umaridadi wa wanafunzi.
.
Mwenyekiti wa mtaa wa Ihumwa A Bw.Wiliamu Njilimuyi amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa tayari umeanza ikiwa vyumba viwili ni nguvu ya wanachi na chumba kimoja ni fedha za Serikali.
.
Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Edwadi Magawa ameeleza jitihada zinazochukuliwa katika ujenzi wa shule mpya utakao saidia kupunguza idadi ya wanafunzi kwa shule mama .INSERT…………………………………………DIWANI
Shule nyingi Nchini zimeendelea kupambana na idadi kubwa ya wanafunzi katika mashule hali inayochangiwa na uandikishwa watoto mashuleni kuongezeka .
.