Dodoma FM

Moto wateketeza maduka Jijini Dodoma

21 January 2025, 6:04 pm

Picha ni harakati za kuzima moto huo zikiendelea katika jiji la Dodoma. Picha na Mariam Kasawa.

hakuna madhara ya kifo yaliyotokea katika ajali ya moto huo.

Na Mariam Kasawa
Takribani maduka 10 yaliyopo katika Barabara ya Nane katikati ya Jiji la Dodoma yameteketa kwa moto uliozuka leo Januari 21, 2025 majira ya saa moja asubuhi, na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa wafanyabiashara wa eneo hilo huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hajajukikana.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Rehema Jeremiah Menda amesema hakuna madhara ya kifo yaliyotokea huku chanzo kikiwa kinaendelea kuchunguzwa licha ya kudhaniwa kuwa ni uchakavu wa miundombinu ya mifumo ya umeme Kwa sababu jengo hilo ni la muda mrefu.

Picha ni Wananchi wakiwa eneo hilo ambalo maduka yameungua moto .Picha na Jambo Tv.
Sauti ya Mrakibu Rehema Jeremiah Menda .

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaji Jabir Shekimweri amefika katika eneo la tukio mapema asubuhi ambapo amezungumzia tukio hilo pamoja na kutoa pole kwa wafanyabishara walio kumbwa na mkasa huo wa moto.

Sauti ya Alhaji Jabir Shekimweri.