Dodoma FM
Wanawake KLPT watakiwa kujitokeza siku ya uchaguzi Nov. 27
29 October 2024, 3:59 pm
Na Noel Steven
Wanawake wa kanisa Kanisa la Pentekoste Tanzania KLPT Wilayani Mpwapwa, wamehimizwa kujitokeza siku ya uchaguzi Novemba 27 Ili kuweza kuchagua viongozi bora wa Serikali za mitaa.
Akiongea katika siku ya kuhitimisha wiki ya wanawake KLPT Parishi ya Ng’ambo, Mch. Beatus Magesa amewataka wananwake hao kujitokeza kupiga kura ili kupata viongozi bora watakaoshika hatamu ya uongozi.
Aidha Jane Isaack Fonga Katibu wa idara ya wanawake kanisani hapo amewataka wanawake kutobaki nyuma kwa suala la uchaguzi.
Mmoja ya mshiriki aliyehudhuria Kongamano hilo lililofanyika Wilayani Mpwapwa Okt. 27, 2024 kuhitimisha wiki ya wanawae KLPT , anaeleza athari za kutojitokeza kwenye chaguzi zijao.