Dodoma FM
Ulinzi na usalama waimarika Mkonze kudhibiti uhalifu, mauaji
9 October 2024, 6:26 pm
Hali ya ulinzi na usalama imeimarika katika kata ya Mkonze kufuatia matukio kadhaa ya mauaji yaliyotokea katika kata hiyo kwa nyakati tofauti miiezi ya hivi karibuni.
Akiongea na Dodoma TV, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani katika kata hiyo Bwn. Sospeter Abel amebainisha hatua waliyoichukua ili kudhibiti mauaji.
Aidha wananchi wa kata hiyo wamesema kwamba hali ya ulinzi na usalama vimeimarika kwa sasa baada ya hatua walizochukua katika kudhibiti matukio ya mauaji yanayojitokeza mara kwa mara hapo awali.