Dodoma FM

Viongozi watarajiwa mjipange kutekeleza hoja za wananchi

4 October 2024, 8:08 pm

Na Lilian Leopold   

Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu, wananchi Mkoani Dodoma wamesema wamepata hamasa  ya kuchagua viongozi sahihi watakaotatua changamoto zao.

Wakizungumza na Dodoma TV baadhi ya wananchi hao wamebainisha kuwa wanatamani viongozi watakaochaguliwa watatue changamoto zinazowakabili ili kuleta maendeleo katika maeneo yao.

Sauti za wanachi

Katika hatua nyingine wananchi wameongeza kuwa viongozi wanapaswa kutembelea maeneno waliyochaguliawa ili kujua changamoto za wananchi wao.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Nchini unatarajia kufanyika Novemba 27 huku wagombea wakitarajiwa kuchukuwa fomu za kugombea Novemba 1-7 Mwaka huu.