Dodoma FM

Wanne mbaroni tuhuma za mauaji Dodoma

30 September 2024, 7:11 pm

Na Nazael Mkude.

Watu wanne wanashikiliwa na  Jeshi la Polisi kwa tuhuma  za matukio ya mauaji yaliyofanyika kwa nyakati  na muda tofauti ndani ya Jiji la Dodoma.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabaz amesema  kuwa maeneo yalikotokea mauaji hayo ni pamoja na Mahomanyika Nzuguni, Mbuyuni Kizota, Mkonze na  Segu Bwawani Nala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bwn. George Katabazi
Sauti ya George Katabazi