Dodoma FM

Serikali kudhibiti wizi wa vifaa vya ujenzi uwanja wa ndege Msalato

24 September 2024, 8:31 pm

Na Mindi Joseph

Udokozi na wizi wa vifaa vya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato Jijini Dodoma umesababisha hasara kwa mkandarasi.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Jabiri Shekimweri anasema serikali haitafumbia macho wizi wa vifaa vya ujenzi uliofanyika katika stoo ya kuhifadhia viafaa ya mkandarasi anayejenga uwanja wa ndegewa kimataifa  Msalato jijini Dodoma.

Mheshimwa Jabir Shekimweri Mkuu wa Wliaya ya Dodoma akiwa eneo la ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato
Sauti ya Mheshimiwa Jabir Shekimweri

Aidha Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Zuhura Amani anasema pamoja na jitihada mbalimbali wanaweka mifumo thabiti ya wizi kutofanyika tena.

Mh. Jabir Shekimweri akiwa kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato
Sauti ya Bi. Mhandisi Zuhura

Ujenzi huo ulioanza  Novemba mwaka 2022 unahusisha sehemu mbili upande wa majengo na miundombinu ambapo sehemu ya ujenzi wa majengo imefikia asilimia 43.6 na Miundombinu  ni asilimia 75.8.

Picha kuonesha taswira ya uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato