Mgogoro wa ardhi Zanka mbioni kutatuliwa
5 September 2024, 8:02 pm
Mbunge wa jimbo la bahi mh Kenneth Nolo mkoan Dodoma amehahidi kumaliza mgogoro wa ardhi unaowakabili wanachi wa kijij cha Zanka
Mgogoro wa ardhi Zanka mbioni kutatuliwa
Na Nazaeli Mkude
Mbunge wa jimbo la Bahi Mhe, Kenneth Nolo Mkoan Dodoma amehahidi kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya wanachi wa kijij cha Zanka na jeshi.
Katika jitihada za kutatua mgooro huo, Mheshimiwa Kenneth Nolo amefanya ziara maalumu ya kuwatembelea wananchi hao na kudokeza kuwa changamoto hiyo imeshajadiliwa katika vikao vya mkoa ikishirikisha Waziri wa ulinzi ili kuhakikisha mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi.
Wananchi wa Kijiji cha Zanka wamedai haki ya umiliki wa maeneo hayo kwa madai kuwa wamekuwa katika maeneo hayo kwa miaka 35 lengo la kuanzisha makazi.