Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari ugonjwa wa macho mekundu
17 January 2024, 7:42 am
Kwa Mujibu wa taarifa hiyo ya Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka wizara ya Afya Profesa Ruggajo Katika kipindi cha Desembe 22, 2023 hadi Januari 11, 2024 kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaosumbuliwa Akitolea Mfano mkoa wa Dar Es Salaam ambapo kuna wagonjwa wapya 869 ambapo ni ongezeko kubwa kwani katika kipindi cha mwezi Desemba 2023 kulikuwa na wagonjwa 17.
Na Fred Cheti.
Serikali kupitia Wizara ya afya siku ya jana iliwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa macho mekundu (Red eyes) Maambukizi ya Kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho ugonjwa ulioibuka nchini hivi karibuni.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof Pascal Ruggajo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa awali ya ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuathiri watu wengi nchini.
Dodoma Tv Imefanya Mahojiano na Daktari bingwa wa Macho kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo amezungumzia dalili za ugonjwa na jinsi unavyoambukizwa huku akitoa wito kwa wananchi kuzingatia usafi kwani ndio njia pekee ya kuzuia maabukizi ya ugonjwa huo.
Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya wananchi jijini hapa ambapo wengi wameonesha kutokua na uelewa na wa kutosha juu ya ugonjwa huo na wameshauri elimu zaidi itolewe kwa jamii juu ya ugonjwa huo