Shule ya msingi Chilanjilizi yalia na uhaba wa walimu wakike
15 November 2023, 3:34 pm
Shule zenye wanafunzi mchanganyiko ni vyema kuwa na walimu wa jinsia zote kwani Watoto wa kike shuleni wanahitaji uangalizi ili kuwapa ujasiri na uwezo wa kueleza matatizo yanayowakuta wasichana wawapo shuleni.
Na Victor Chigwada
Wananchi wa Kata ya Ngomai wilayani Kongwa wameiomba Serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa pamoja na walimu wa jinsia ya kike kwa shule ya msingi chilanjilizi.
Wakizungumza na Taswira ya habari kwa Nyakati tofauti wamesema kuwa licha ya uchache wa vyumba vya madarasa pia wana changamoto ya uhaba wa walimu wa jinsia ya kike kwa kwa shule ya msingi
Aidha shule hiyo inakabiliwa na adha ya maji kama ambavyo Mwenyekiti wa mtaa wa kawawa Bw.Sospita Njamai anabainisha changamoto hiyo.
Akizungumza Hali ilivyo ya Shule hiyo Diwani wa Kata hiyo Bw.Martini Mwidimila amesema ni kweli shule hiyo ina uhaba wa walimu wa kike pamoja na walimu wa masomo ya hisabati kwa upande wa sekondari