Ugumu wa maisha watajwa kuwa sababu ya watu kujiua
13 September 2023, 3:27 pm
Septemba 10 kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya kuzuia kujiua ambapo Kitaifa maadhimisho hayo yalifanyika katika Hospitlai ya Taifa ya akili Mirembe jijini Dodoma.
Na Katende Kandolo.
Imeelezwa kuwa ugumu wa maisha pamoja na msongo wa mawazo ni miongoni mwa sababu inayopelekea baadhi ya watu kujiua.
Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa katika maeneo mbalimbali duniani.
Kufuatia suala hilo Dodoma Tv imefanya mahojino na baadhi ya wananchi jijini Dodoma ambapo kwanza nilianza kwa kuwauliza je ni ipi sababu inayosababisha baadhi ya watu kuchukua maamuzi ya kujiua?
Septemba 10 mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya kuzuia kujiua Duniani yaliyofanyika katika hospitali ya Taifa ya akili Mirembe jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju alieleza kuwa changamoto ya malezi na makuzi ni chanzo kwa baadhi ya watu kuamua kujinyonga kwa kukosa ustahimilivu na mbinu sahihi za kukabiliana na changamoto ya maisha.