Wananchi watakiwa kufahamu umuhimu wa Parachichi
14 August 2023, 6:25 pm
Kwa mujibu wa Jarida la Jumuiya ya Moyo la Amerika linaelezea kuwa kula Parachichi kunaweza kupunguza hatari ya Ugonjwa wa Moyo na Mishipa kulingana na utafiti mpya uliochapishwa hivi karibuni.
Na Abraham Mtagwa.
Wananchi Jijini Dodoma wameshauriwa kuwa watumiaji wazuri wa tunda la Parachichi kwani lina faida nyingi kiafya.
Akizungumza na Taswira ya Habari leo, Bw.Stephano Daburu ambaye ni Mteknolojia na Mtaalamu wa Afya amesema kuwa, tunda la Parachichi ni moja ya matunda muhimu yenye kazi nyingi na faida kubwa katika mwili wa binadamu tofauti na mitazamo ya Watu wengi .
Aidha Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya watumiaji wa Parachichi wanaoishi Jijini Dodoma ambao wamekiri kunufaika na tunda hilo huku wakibainisha matumizi mbalimbali na faida zake katika mwili wa Binadamu.
Vilevile tumezungumza na Baadhi ya Wafanyabiashara wa Parachichi katika soko kuu la Majengo Jijini Dodoma, kujua hali ya soko la Parachichi na muitikio wa wananchi katika kununua tunda hilo.