Wakulima wapongeza mfumo wa M-KULIMA
7 August 2023, 2:52 pm
M-Kulima ni mfumo unaolenga sekta ya kilimo na unatumika mahali popote kwa mkulima kupokea malipo yake kwa wakati na unarahisisha shughuli za Kilimo.
Na Mindi Joseph.
Wakulima wa zao la Zabibu Mkoani Dodoma wamepongeza uwepo wa mfumo wa M-kulima kwani unamrahisishia Mkulima kupokea malipo yake na kuhakikisha pesa yake inakuwa salama.
Teknolojia hii imeongeza Tija kwa wakulima kupokea malipo yao kwa wakati kupitia mfumo wa M-kulima.
Wakulima wanasema M-kulima imeondoa changamoto za ukosefu wa taarifa muhimu za Kilimo.
Mratibu wa M-kulima Kanda ya Kati Robert Mbata amesema lengo la kuwaalika wakulima katika Banda lao Nanenane ni kutoa elimu ya Kutumia Mfumo huo unaomrahisishia mkulima kupokea malipo yake na kuhakikisha pesa yake inakuwa salama.