Mradi wa maji Nzuguni sio porojo, wafika asilimia 76
28 July 2023, 4:48 pm
Mradi wa Nzuguni unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita mlioni 68.7 mpaka milioni 76.3 kwa siku sawa na ongezeko la 11.4% ya uzalishaji wa sasa, na litapunguza mahitaji kwa 11.7% ya mahitaji ya sasa ya lita 133.4 milioni kwa siku.
Na Seleman Kodima.
Mamlaka la Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma DUWASA imesema mradi wa uchimbaji wa visima vya maji katika eneo la Uzunguni umefikia asilimia 76 huku utekelezaji wake ukiendelea katika eneo hilo
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph wakati akitoa taarifa ya huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa waandishi wa habari ambapo amesema mradi wa Nzuguni upo kwenye utekelezaji ambapo katika awamu ya kwanza kiasi cha shilingi bilioni 4 .8 zinatekeleza mradi huo.
Aidha amesema DUWASA inaendelea na utafiti, kuchimba na kuendeleza visima maeneo ya pembezoni mwa mji , lengo la mpango huu ni kupunguza adha kwa wakazi katika maeneo hayo, na kupunguza utegemezi wa chanzo kikubwa cha Mzakwe, wakati wanasubiri uwekezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati jijini Dodoma.
Akizungumzia Uchimbaji Visima pembezoni mwa Mji ili kupata vyanzo vingine vya maji kwa wakazi wa Jiji la Dodoma Mhandishi Aron amesema kuwa milioni 664 zinatatumika kwa ajili kuchimba visima 15 katika maeneo ya mbalimbali ya pembezoni mwa mjini ambapo tayari DUWASA imeingia mkataba na mkandarasi kampuni ya PNR Drilling Company kwa ajili ya shughuli hiyo
Mhandisi Aron amewahakikishia wakazi wa Dodoma kuhusu Miradi ya muda mfupi hatakawia kuisha ambapo mradi wa mfupi ambao utachukua muda mrefu ni wa Zuzu -Nala ambao unatarajiwa kukamilika December 2024.
Kwa upande wa huduma ya usafi wa mazingira (majitaka) DUWASA Mhandisi Aron amesema wanaendelea kuwahudumia wakazi wa mjini Dodoma kwa wastani wa 20% Huku Sehemu kubwa inayohudumiwa ni mjini kati na maeneo machache ya pembezoni kama Kikuyu, Area A, Iringa Road, na Kizota.
Aidha amesema mradi wa ukarabati wa Mfumo wa Majitaka Area C na D jijini Dodoma wenye thamani Bilioni 4. 956 umefika asilimia 89.7% za utekelezaji ambapo Kukamilika kwa mradi huo kutaondoa adha ya harufu kali, kufurika na kutapakaa mara kwa mara, kwa majitaka katika maeneo ya area C na D.